Monday, May 12, 2014

BOKO HALAMU WAONYESHA WASICHANA WALIOTEKA


Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria wataachiliwa huru.
image
Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo, kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.
Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake miamoja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.
Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram.

Wednesday, May 7, 2014

MAGARI ZAIDI YA MIA YAKWAMA ENEO LA MANZESE BARABARA YA DAR ES SALAAM MTWARA


 Malori na Mabasi yakiwa kwenye msururu mrefu mara baada ya kushindwa kuendelea na safari kwa takribani masaa zaidi ya nane katika eneo la Manzese lililopo Kilwa barabara ya Dar Es salaam kuelekea Mtwara hapo jana kutokana na eneo hilo kuharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha na kupelekea magari zaidi ya mia kukwama
 Baadhi ya wasafiri kwenye mabasi yaendayo Dar Es Salaam kutoka Mtwara, Lindi na Kilwa na yale yatokayo Jijini Dar Es Salaam kuekelea mikoa ya Kusini wakiwa wamesimama
kushuhudia juhudi zinazofanya na vijana wa eneo la Manzese na baadhi ya madereva wa malori na mabasi pamoja na abiria kuhakikisha wanasaidia magari kuvuka ili kuweza kuendelea na safari zao.
 Wasafiri na wakazi wa Eneo la Manzese wakishuhudia greda lililofika kwaajili ya kusaidia kusawazisha eneo hilo na kutoa magari yaliyonasa kutokana na eneo hilo kujaa maji na tope zito yaliyosababisha magari kukwama kwa takribani masaa zaidi ya nane hapo jana.
 Mabasi yatokeayo Mikoa ya Kusini kuelekea Bara yakiwa yamekwama katika eneo la Manzese - Kilwa kutokana na barabara kuwa mbovu katika eneo hilo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kupelekea kusababisha magari zaidi ya mia kunasa na kutoendelea na safari zao kwa zaidi ya masaa nane.

Greda likiondoa tope na kusawazisha eneo hilo ambalo lilileta usumbufu mkubwa sana kwa watumiaji wa barabara ya Dar Mtwara na kupelekea magari zaidi ya mia kukwama katika eneo hilo lililoaharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha. 
 Malori yakiwa kwenye msururu.
(Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog)

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSINA NA VURUGU ZILIZOTOKEA DODOMA:


nomaaa
Kutoka Dodoma Mei 05 majira ya saa saba mchana kulitokea vurugu zilizoanzishwa na wabeba mizigo wa Mji mdogo wa Kibaigwa ambapo taarifa inasema zilikua ni vurugu zilizosababisha magari kadhaa kuvunjwa vioo.
Miongoni mwa magari yaliovunjwa vioo ni pamoja na la Mbunge wa Tanga Omary Nundu,gari la Polisi na basi linalofanya safari zake kati ya Dar na Mwanza la Shabaha mbali na kuvunjwa kwa magari hayo pia maduka yaliporwa na hata barabara kuu ya Dodoma-Morogoro ilifungwa.
misimeee
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma amesema David Misime amesema Mpaka sasa jeshi la polisi linawashikiliwa watu 34 ambao ni wakazi wa kibaigwa kata ya kibaigwa wilaya ya kongwa kwa makosa ya kufanya fujo na kuharibu mali

Monday, May 5, 2014

MABASI MAWILI YALIPUKA KENYA


Watu wawili wameuawa na wengine 60 kujeruhiwa kufuatia milipuko miwili katika mji mkuu wa Kenya Nairobi ambayo imelenga mabasi mawili ya abiria.
Mabasi hayo yalilipuliwa katika eneo la barabara ya Thika karibu na mji mkuu.

Mlipuko mmoja umetoa katika basi la abiria ambalo lilikua likisafirisha abiria kutoka mjini Nairobi katika barabara ya Thika ambayo kawaida ina shughuli nyingi.
Basi la pili lililipuliwa karibu na hoteli moja iliyo umbali wa dakika chache kutoka jengo kubwa zaidi la maduka katika katika eneo hilo.
Shughuli za uokoaji zinaendelea na bado hakuna taarifa rasmi kuhusiana na watu waliouawa au kujeruhiwa kwa jumla. Picha za televisheni zinaonyesha mabasi hayo yakiwa yameharibiwa na madirisha kuvunjika.
Ni hapo jana tu ambapo watu wanne waliuawa na wengine wapatao ishirini kujeruhiwa katika shambulio lingine ambapo grunedi ilirushwa katika kituo cha mabasi ya abiria.
Shambulio la pili lilitokea karibu na mkahawa mmoja maarufu lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Mashambulio haya yanatokea mwezi mmoja tu baada ya serikali kuanzisha oparesheni ya usalama baada ya kukumbwa na mashambulio mengine hapo awali na pia kupata vitisho kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Alshabab waliodai kutekeleza shambulio la Westgate ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa.