Sunday, April 27, 2014

WAZIRI MKUU WA KOREA KUSINI AJIUZULU



 
Waziri mkuu wa Korea Kusini Chung Hong-won amejiuzulu kufuatia kuzama kwa Ferry ya Sewol iliyokuwa na jumla ya abiria 476 wengi wao wakiwa ni wanafunzi na walimu, huko pwani ya kusini ya nchi hiyo wiki iliyopita.
“vilio cha familia za wale ambao bado hawajaonekana vinanikosesha usingizi usiku” alisema Chung Hong-won.
Maafisa wa Korea Kusini wamethibitisha jumla ya watu 187 walipoteza maisha katika ajali hiyo.
Wakati akitoa taarifa ya kujiuzulu alisema kitu sahihi anachotakiwa kufanya sasa ni kuwajibika na kujiuzulu kutokana na kile kilichotokea, na kuomba radhi kwa niaba ya Serikali.
image
Baadhi ya wakazi wa Korea Kusini wakimtazama Waziri mkuu wakati akijiuzulu
Haya ndio maneno ya Mr Chung aliyoyasema kupitia televisheni:
“The right thing for me to do is to take responsibility and resign as a person who is in charge of the cabinet, on behalf of the government, I apologise for many problems from the prevention of the accident to the early handling of the disaster.”
image
Aliongeza: “There have been so many varieties of irregularities that have continued in every corner of our society and practices that have gone wrong. I hope these deep-rooted evils get corrected this time and this kind of accident never happens again.”
Rais Park Geun-hye wa Korea Kusini amekubaliana na kujiuzulu wa waziri mkuu wake.
Source: BBC

Thursday, April 24, 2014

MAIGE "KUWA NA SEREKALI TATU TANZANIA ITAINGIA KATIKA MAAJABU YA DUNIA"

Mjumbe wa Bunge la Katiba, Almas Maige amesema endapo wajumbe wa Bunge hilo watapitisha muundo wa Serikali tatu, nchi itaingia katika kitabu cha maajabu ya dunia cha Guiness Book of Records.

“Hili litakuwa shirikisho la pekee hapa duniani lenye marais wengi katika nchi mbili, linaweza kuingia katika kitabu cha maajabu cha Guiness kwa kuwa na marais wengi katika nchi maskini sana,” alisema.

Mjumbe huyo alisema amejaribu kufuatilia hoja za wanaounga mkono muundo huo na kufananisha na nchi za Marekani na Nigeria, lakini akasema katika nchi hizo Rais wa nchi ni mmoja.

“Mimi nimejaribu kuwafuata wanaofananisha na Marekani na Nigeria, wameshindwa kusema katika nchi hizo mbili Rais ni mmoja tu hakuna wingi wa Rais kutokana na majimbo,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, mjumbe huyo aliwashangaa wajumbe wanaotokana na kundi la Ukawa kujigeuza kuwa wachunguzi wa kijinai kwa kuhoji uhalali wa saini ya muasisi wa Muungano, Abeid Aman Karume.

“Mimi nawashangaa sana wanasiasa hawa na wanasheria wa Ukawa wamejigeuza Forensic Expert (wachunguzi wa jinai). Mimi ningewaunga mkono kama wangeenda kuwauliza watoto wa marehemu,” alisema.

Aliongeza kusema: “Watoto wa marehemu wapo Zanzibar… Yupo Aman Karume aliyekuwa Rais wa Zanzibar na yuko Balozi Ali Karume na yuko pia mama Karume. Kwa nini hawawaulizi,” alihoji.

“Mimi ningefurahi sana kama wangeenda kuwauliza wanafamilia sahihi hii ni ya baba yenu? Au je, mheshimiwa mama hii ni sahihi ya mumeo? Wangekataa ndipo tungewaunga mkono,” alisisitiza.

Mjumbe huyo alisema kinyume chake, Ukawa wanavaa gamba la elimu ambayo hawana na vilevile hawajui maana na tafsiri sahihi iliyoandikwa miaka 50 iliyopita.

“Taaluma ya sasa ingeweza kugundua wino uliotumika una umri gani na kuondoa kero hiyo kama ni ya juzi au jana au kama imeghushiwa,” alisema mjumbe huyo na kuongeza kusema:

“Wataalamu wa Forensic (uchunguzi wa kijinai) wangeweza kugundua wino huo una miaka 50. Wanafanya kitu ambacho hawakijui na wanadhalilisha Watanzania.”

Mjumbe huyo alisema yeye anaunga mkono muundo wa Muungano wa Serikali mbili na kuwa Serikali tatu ni sawa na mtu kunywa sumu.

Tuesday, April 22, 2014

HISTORIA YA MUUNGANO WA TANZANIA APRIL 26 MWAKA 1964


Historia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaanzia April 26 mwaka 1964 siku ambayo Nchi ya Jamuhuri ya Tanganyika ambayo kwa sasa ni Tanzania bara pamoja na iliyokuwa Jamuhuri ya Zanzibar (inayojumuisha Visiwa vya Pemba na Unguja) ziliungana na kuwa nchi moja.
Kumbu kumbu zinaonyesha Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ziliingia mkataba tarehe 22 Aprili 1964 huko Zanzibar kwa lengo la kuunganisha nchi hizo mbili baada ya kutiwa saini na viongozi wa nchi hizo kwa wakati huo ambao ni aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.
Baada ya kutiwa saini kwa mkataba huo au kama unavyojulikana hati ya Muungao baadae makataba huo ulipelekwa kwenye mabunge yote mawili yaani Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi tarehe 26 Aprili, 1964 ili uridhiwe rasmi kuwa sheria ya Muungano ambapo nchi mpya inayojulikana “Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar” ilizaliwa ambapo sherehe kubwa zilizofana za kuchanganya udongo wa pande zote mbili zilifanyika ili ku.
Hata hivyo nchi hii mpya iliendelea kujulikana kwa jina hilo la”Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar” hadi Oktoba 28, 1964 lilibadilishwa rasmi kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jina linatumika hadi hivi leo kupitia Sheria ya Jamhuri ya Muungano, Sheria namba 61 ya mwaka 1964.
Kwa ujumla Muungano huo wa kuunganisha nchi mbili kwa hiari umekuwa ukisifiwa kwamba ni Muungano wa kipekee barani Afrika Professa Paramagamba Kabudi Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yeye anasema katika utafiti wake amegundua ni Muungano huo ndio pekee wa hiari uliodumu hadi hivi leo.
Muundo wa Muungano uliokubaliwa
Nchi mpya iliyozaliwa yaani Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni muungano wenye Muundo wa vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji ambavyo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Pia vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki ambavyo ni Mahakama ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
na pia vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma ambavyo ni Bunge la Jamuhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi.
Katika utekelezaji wa shughuli zake Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenyewe imepewa mamlaka ya kushughulikia mambo yote ya Muungano kama yalivyoainishwa katika Katiba ya Tanzania na mambo yale yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Bara huku Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenyewe imepewa mamlaka ya kushughulikia mambo yote yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Zanzibar.
Mambo ya Muungano
Mambo ya Muungano ya kwanza kabisa yaliyoanishwa kwenye Katiba ya muda ya mwaka 1965 yalikuwa ni 11 ambayo ni
• Katiba na Serikali ya Muungano
• Mambo ya Nchi za Nje
• Ulinzi
• Polisi
• Mamlaka juu ya mambo yanohusika na hali ya hatari
• Uraia
• Uhamiaji
• Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje
• Utumishi katka Serikali ya Jamhuri ya Muungano
• Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,
ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa
nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
• Bandari mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na
simu.
Hata hivyo Baadae Mambo ya Muungano yaliongezeka kutoka kumi na moja (11) hadi ishirini na mbili (22)
Likiwemo suala la sarafu na benki kuu ambapo nchi zote zilianza kutumia sarafu moja hadi hivi leo.
Mbali na mafanikio yaliyopatikana Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar umekuwa ukipitia safari ya mabonde na malima ambapo wapo wanaona kuwa umewapa manufaa huku wengine wakidhani muungano hauna faida.
Kwa sasa Tanzania ipo kwenye mchakato wa kuandika Katiba Mpya ambapo suala la Muundo upi wa Muungano unaofaa kati ya Muundo uliopendekezwa kwenye rasimu ya Katiba wa serikali tatu na muundo wa sasa unaopigiwa debe na chama tawala wa serikali mbili ni mjadala uliopamba moto katika nchi hii.
Hata hivyo kwa vyovyote vile pamoja na changamoto na matatizo yote hayo ni wazi muungano huo kufikisha miaka 50 sio jambo dogo.

Thursday, April 17, 2014

AKAMATWA NA KILO 10 ZA MADAWA YA KULEVYA (HEROIN) AKITOKEA TANZANIA

Mfanyabiashara mwanamke wa Kighana (pichani) amekamatwa na kilo 10 za Heroin wakati akitokea Tanzania. Mercy Agyeman Prempeh (36) amekamatwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kotoka wakati akitokea Tanzania.


Polisi walimtaka mwanamke huyo kutambua mizigo yake uwanjani kutokana na sehemu aliyokuwa anatokea yaani Tanzania.
Baada ya kuhojiwa na polisi alidai kuwa rafiki yake wa Kitanzania ndiye aliyempa mzigo huo ampelekee mtu asiyejulikana anayeishi katika jiji la Accra kwa ada ya Dola za Kighana 2,500. Amedai mwenye mzigo alitakiwa akutane nae hapo airpot na kumpatia kiasi hicho cha fedha lakini anaamini amengia mitini baada ya yeye kukamatwa.

WATU 3 MBARONI KWA KUKUTWA NA BANGI NDANI YA BASI


 Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia abiria wa tatu waliokuwa wakisafiri na Basi la New Force kutoka Kahama kuelekea Jijini Dar es Salaam.Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime, wamekamatwa leo mchana wakiwa wanasafirisha Debe ishirini za bangi.

Wanaoshikiliwa ni Kevin Prospar(aliyekaa pichani kulia),Joseph Charles (aliyekaa kulia) na John Joseph(aliye kaa katikati)
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime kushoto akikagua bangi iliyo kamatwa.
Basi la New Force lililokamatwa likiwa limebeba abiria waliokuwa na bangi likiwalimeshililiwa kwa muda Makao ya Polisi Mkoa wa Dodoma

Tuesday, April 15, 2014

MTAA WA WATANZANIA WAISHIO AFRICA KUSINI WAVAMIVA KWA KUCHOMEWA VITU PAMOJA NA KIPIGO

MTAA WA WATANZANIA AFRICA KUSINI WAVAMIWA NAKIPIGO JUU

Afrika Kusini ni nchi yenye uchumi mkubwa Afrika,na Waafrika wengi hukimbilia huko kwa ajili ya kufanya kazi kama za Udereva, uuzaji mafuta kwenye vituo vya mafuta pamoja na kazi nyingine mbalimbali.

Taarifa kutoka kwenye mji wa Pretoria ni kwamba Watanzania ambao wanamiliki na kufanya biashara mbalimbali zikiwemo za Maduka na wale wanaomiliki hoteli, wamevamiwa wakiwa kwenye malizao na kufanyiwa uharibifu na nyingine kuchomwa moto.

Ni kundi la watu ambalo linaendeleza uvamizi huu ambapo linawashutumu Watanzania kuhusika na biashara ya dawa za kulevya. Inaaminika kuwa kundi hili lina sehemu kubwa ya madereva Taxi wazawa wa nchi hiyo ambao wamekua wakiumizwa na jitihada za raia wa kigeni wa Nigeria na Watanzania ambao wamejazana kwenye mtaa wao wakimiliki maduka mbalimbali yakiwemo ya nguo pamoja na hoteli.

Tayari balozi wa Tanzania amekutana na Watanzania hao na kuahidi kulifatilia suala hilo,ambapo Watanzania watano wamejeruhiwa wakiwemo watatu ambao bado wako hospitali na mmoja wao kavunjika mkono, mmoja kapigwa kichwani.
Kabla ya Watanzania wengine kuwahi kufunga maduka yao, maduka matatu ya Watanzania pamoja na hoteli mbili zinazomilikiwa na Watanzania zilivamiwa na wakachuchukuliwa simu na watu kupigwa ambapo polisi walipokuja hakuna chochote kilichofanyika zaidi ya maelezo.Picha hizi zote zilipigwa na Mtanzania akiwa anakimbia baada ya kufanikiwa kufunga duka lake.

SAMWELI SITTA-”KUANZIA SASA TBC1 WAKIKATA MATANGAZO HATUWEZI KUKATISHA KUENDELEA NA BUNGE”


SITTA-”KUANZIA SASA TBC1 WAKIKATA MATANGAZO HATUWEZI KUKATISHA KUENDELEA NA BUNGE”Jumamosi iliyopita matangazo ya Television ya taifa yalikatika wakati ikiwa live kwenye bunge la katiba ambapo Mh. Tundu Lissu alikua akiwasilisha maoni ya wachache ambako kulisababisha Mwenyekiti kuahirisha bunge hilo mara moja baada ya kugundulika hawakuwa wanaonekana live.

Kukatika huko kwa matangazo ambako badae kulitangazwa kwamba ni kutokana na hali ya hewa kulifanya TBC itupiwe lawama au malalamiko yakiwemo kutoka kwa baadhi ya viongozi na Wananchi huku baraza la habari likisema ni kitendo cha aibu na watafatilia kujua kama ni kweli hali ya hewa au hujuma.

Baada ya hayo yote na kauli zilizotolewa na Wanasiasa mbalimbali baadae, Samwel Sitta ambae ni Mwenyekiti wa bunge la katiba hapa 104.4 Dodoma ametoa taarifa rasmi akisema >> ‘kuanzia sasa matangazo ya live bungeni TBC1 yakikatika hatutawezi kukatisha kuendelea na bunge’
‘Tunazingatia kwamba ipo Radio na Wananchi wengi wa Tanzania wanasikiliza radio na mtu mwenye TV hawezi kushindwa kununua radio kwa hiyo hatuwezi kukatiza kila wakati, ikiwa radio inaendelea kazi yetu humu ndani itaendelea’ – Samwel Sitta

WANAFUNZI 200 WATEKWANYARA NIGERIA


WANAFUNZI 200 WATEKWANYARA NIGERIA
Shambulizi hili linadaiwa kufanywa na Boko Haram ingawa kundi hilo halijakiri kulitekeleza.Polisi nchini Nigeria wanasema kuwa shule ya mabweni ya wasichana imeshambuliwa katika jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Wazazi wanasema kuwa zaidi ya wasichana miambili wametekwa nyara na washambuliaji hao.

Washambuliaji wanaaminika kuwa wanachama wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram.
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa wanajeshi wawili waliuawa huku mali ikiharibiwa wakati wa shamblizi hilo mjini Chibok.
Mnamo siku ya Jumatatu, zaidi ya watu 70, waliuawa katika milipuko miwili ya mabomu katika kituo cha mabasi mjini Abuja.
Kundi la Boko Haram pia limelaumiwa kwa kufanya shambulizi hilo.

Thursday, April 10, 2014

BILLIONAIRE WA MAREKANI ‘HOWARD BUFFET’ ATEMBELEA MBUGA ZA TANZANIA


BILLIONAIRE WA MAREKANI ‘HOWARD BUFFET’ ATEMBELEA MBUGA ZA TANZANIA
Billionaire wa Marekani Howard Buffett atembelea Serengeti National Park na Ngorongoro Crater kwa siku tatu za likizo yake baada ya kuvutiwa sana na vivutio vya utalii wa Tanzania alipotembelea nchi hii mwezi uliopita.

Wakati wa ziara yake ya mwisho nchini mwezi Machi mwaka huu , Howard Buffett ambaye ana shauku ya uhifadhi wa mazingira kupitia mfuko Howard Buffett Foundation alichangia helikopta mbili kwa Serikali ya Tanzania kutumika kwa ajili ya shughuli za kupambana na ujangili katika maeneo ya hifadhi.

Katika Kilimanjaro International Airport, Buffett akiongozana na mkewe alipokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu .

Howard Buffett ngoma na Wamasai Utamaduni Group katika KIA .
http://www.baabkubwamagazine.com/wp-content/uploads/2014/04/image93.jpg
Ghoosh …. i unaweza pia kuruka juu kama Wamasai … Buffett anaonekana kusema hivyo.

Hebu angalia ambao wanaweza kuruka juu …

Howard Buffett akicheza ngoma na wanawake wa Kimasai.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu inatoa ruzuku ya paa kwa Howard Buffett .

BIG UP na moja ya Rangers Park katika KIA .
Picha zote na Pascal Shelutete , TANAPA

WAZIRI MEMBE KUPOKEA TUZO YA AFRICA’S MOST IMPACTFUL LEADER OF THE YEAR KWA NIABA YA RAIS KIKWETE

WAZIRI MEMBE KUPOKEA TUZO YA AFRICA’S MOST IMPACTFUL LEADER OF THE YEAR KWA NIABA YA RAIS KIKWETE Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) atapokea tuzo ya Africa’s Most Impactful Leader of the Year kwa niaba ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania mjini Washington D.C, Marekani tarehe 09 Aprili, 2014.

Tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka na Taasisi ya Uchapishaji ya African Leadership Magazine yenye makazi yake nchini Marekani kwa viongozi wa Afrika wanaofikia vigezo vilivyowekwa na Taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuzingatia utawala bora, demokrasia na kuheshimu haki za binadamu kwa Mwaka 2013 inatolewa kwa Mhe. Rais Kikwete.

Kwa mujibu wa Taasisi ya African Leadership Magazine, Tuzo hiyo inatolewa kwa Mhe. Rais Kikwete kutokana na namna ya pekee ya uongozi wake wenye matokeo yanayopimika kiutawala bora hususan kwa mwananchi wa kawaida wa Tanzania. Aidha, uongozi wake umeiletea Tanzania heshima kubwa kimataifa na kuiweka Tanzania kama chaguo muhimu kwa wawekezaji kutokana na ukuaji uchumi na maboresho ya sera.
Tuzo hiyo tayari imewahi kutolewa kwa Marais na Viongozi wengine mbalimbali wa Afrika wakiwemo Mhe. Ellen Johnson Sirleaf, Rais wa Liberia, Mhe. James Michel, Rais wa Shelisheli na Rais Mstaafu wa Ghana, Mhe. John Kuffor.
Ujumbe wa Mhe. Membe utamhusisha Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Salvatory Rweyemamu, Waandishi wa Habari na Maafisa wa Serikali. Mhe. Membe atarejea nchini tarehe 11 Aprili, 2014.
Imetolewa na: KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.