Featured Posts Coolbthemes

Monday, June 2, 2014

MLIPUKO WAUA 14 NIGERIA



Polisi Kaskazini mashariki mwa Nigeria
wanasema kuwa shambulizi la bomu limewauwa zaidi ya watu 14 na kuwajeruhi wengine wengi.
Ripoti zimesema kuwa mlipuko huo uliotokea katika mji wa Mubi, ulilenga chumba kimoja cha burudani ambako watu walikuwa wakitazama mechi ya soka kwenye televisheni.
Katika miezi michache iliyopita, Boko Haram wamezidisha mashambulio yao hasa kaskazini mashariki mwa Nigeria. Mamia ya watu wameuawa na wengine wengi kujieruhiwa.
Pia wameshambulia nyumba za watu na kuzichoma moto, na kisa kilicho tikisa jamii ya kimataifa ni wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara yapata miezi miwili sasa hadi leo hawajulikani waliko.
‘Uharibifu uliozidi’
Uharibifu mkubwa wa mashambulio
Mashambulio haya yameacha uharibifu mkubwa. Waliosalimika wamelazimika kukimbia makwao huku shule zikiachwa bila wanafunzi.
Shambulio hilo limetokea karibu na mpaka kati ya Nigeria na Cameroon katika jimbo la Adamawa-mojawepo ya majimbo ambako sheria ya hali ya hatari inatumika kutokana na mashambulizi ya kundi la waislamu wenye itikadi kali la Boko Haramu.
Katika mwezi mmoja pekee watu zaidi ya 200 wameuawa katika mji huo.
Lakini sasa katika maeneo mengine ya kaskazini ambako inasemekana usalama umerejea kiasi, kama vile mji wa Kano juhudi zinafanywa kung’oa mizizi ya uovu huo.
Wanamgambo wa kiislamu AL shabaab wanaodaiwa kuwa na uhusiano na AL qaeda wamekuwa wakiwazuia wananchi kushiriki mambo yanayohusishwa na Mataifa ya magharibi. Inakisiwa kuwa zaidi ya wanafunzi milioni 11 kaskazini mwa Nigeria hawapewi mafunzo mengine yoyote mbali na ya kidini.
Mashirika ya kijamii hasa kutoka Uingereza yamekuwa yakifadhili kupitia taasisi za nchini humo masomo ya ziada hasa katika shule za mafunzo ya kidini, ili yatoe elimu ya ziada mbali na Qurani.
Tayari maelfu ya wanafunzi wanafaidi lakini bado kuna wengi zaidi wanaotishiwa usalama wao na inadaiwa ni kiasi kikubwa zaidi ya nchi hiyo haiwezi kufikiwa.
Licha ya mauaji ya miaka mingi yaliyofanywa na kundi hilo la Boko Haram na hata kujitangaza hadharani uhusiano wao na kundi la AL Qaeda, ni wiki iliyopita tu ambapo Umoja wa Mataiifa umeilitangaza kuwa kundi la kigaidi.
Japo wengi wanaona kuwa hatua hiyo imechelewa, bado inatoa matumaini ya kuweza kuchukuliwa hatua zaidi kusaidia kukabiliana na kundi hilo.

Monday, May 12, 2014

BOKO HALAMU WAONYESHA WASICHANA WALIOTEKA


Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria wataachiliwa huru.
image
Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo, kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.
Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake miamoja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.
Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram.

Wednesday, May 7, 2014

MAGARI ZAIDI YA MIA YAKWAMA ENEO LA MANZESE BARABARA YA DAR ES SALAAM MTWARA


 Malori na Mabasi yakiwa kwenye msururu mrefu mara baada ya kushindwa kuendelea na safari kwa takribani masaa zaidi ya nane katika eneo la Manzese lililopo Kilwa barabara ya Dar Es salaam kuelekea Mtwara hapo jana kutokana na eneo hilo kuharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha na kupelekea magari zaidi ya mia kukwama
 Baadhi ya wasafiri kwenye mabasi yaendayo Dar Es Salaam kutoka Mtwara, Lindi na Kilwa na yale yatokayo Jijini Dar Es Salaam kuekelea mikoa ya Kusini wakiwa wamesimama
kushuhudia juhudi zinazofanya na vijana wa eneo la Manzese na baadhi ya madereva wa malori na mabasi pamoja na abiria kuhakikisha wanasaidia magari kuvuka ili kuweza kuendelea na safari zao.
 Wasafiri na wakazi wa Eneo la Manzese wakishuhudia greda lililofika kwaajili ya kusaidia kusawazisha eneo hilo na kutoa magari yaliyonasa kutokana na eneo hilo kujaa maji na tope zito yaliyosababisha magari kukwama kwa takribani masaa zaidi ya nane hapo jana.
 Mabasi yatokeayo Mikoa ya Kusini kuelekea Bara yakiwa yamekwama katika eneo la Manzese - Kilwa kutokana na barabara kuwa mbovu katika eneo hilo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kupelekea kusababisha magari zaidi ya mia kunasa na kutoendelea na safari zao kwa zaidi ya masaa nane.

Greda likiondoa tope na kusawazisha eneo hilo ambalo lilileta usumbufu mkubwa sana kwa watumiaji wa barabara ya Dar Mtwara na kupelekea magari zaidi ya mia kukwama katika eneo hilo lililoaharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha. 
 Malori yakiwa kwenye msururu.
(Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog)

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSINA NA VURUGU ZILIZOTOKEA DODOMA:


nomaaa
Kutoka Dodoma Mei 05 majira ya saa saba mchana kulitokea vurugu zilizoanzishwa na wabeba mizigo wa Mji mdogo wa Kibaigwa ambapo taarifa inasema zilikua ni vurugu zilizosababisha magari kadhaa kuvunjwa vioo.
Miongoni mwa magari yaliovunjwa vioo ni pamoja na la Mbunge wa Tanga Omary Nundu,gari la Polisi na basi linalofanya safari zake kati ya Dar na Mwanza la Shabaha mbali na kuvunjwa kwa magari hayo pia maduka yaliporwa na hata barabara kuu ya Dodoma-Morogoro ilifungwa.
misimeee
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma amesema David Misime amesema Mpaka sasa jeshi la polisi linawashikiliwa watu 34 ambao ni wakazi wa kibaigwa kata ya kibaigwa wilaya ya kongwa kwa makosa ya kufanya fujo na kuharibu mali

Monday, May 5, 2014

MABASI MAWILI YALIPUKA KENYA


Watu wawili wameuawa na wengine 60 kujeruhiwa kufuatia milipuko miwili katika mji mkuu wa Kenya Nairobi ambayo imelenga mabasi mawili ya abiria.
Mabasi hayo yalilipuliwa katika eneo la barabara ya Thika karibu na mji mkuu.

Mlipuko mmoja umetoa katika basi la abiria ambalo lilikua likisafirisha abiria kutoka mjini Nairobi katika barabara ya Thika ambayo kawaida ina shughuli nyingi.
Basi la pili lililipuliwa karibu na hoteli moja iliyo umbali wa dakika chache kutoka jengo kubwa zaidi la maduka katika katika eneo hilo.
Shughuli za uokoaji zinaendelea na bado hakuna taarifa rasmi kuhusiana na watu waliouawa au kujeruhiwa kwa jumla. Picha za televisheni zinaonyesha mabasi hayo yakiwa yameharibiwa na madirisha kuvunjika.
Ni hapo jana tu ambapo watu wanne waliuawa na wengine wapatao ishirini kujeruhiwa katika shambulio lingine ambapo grunedi ilirushwa katika kituo cha mabasi ya abiria.
Shambulio la pili lilitokea karibu na mkahawa mmoja maarufu lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Mashambulio haya yanatokea mwezi mmoja tu baada ya serikali kuanzisha oparesheni ya usalama baada ya kukumbwa na mashambulio mengine hapo awali na pia kupata vitisho kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Alshabab waliodai kutekeleza shambulio la Westgate ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa.

Sunday, April 27, 2014

WAZIRI MKUU WA KOREA KUSINI AJIUZULU



 
Waziri mkuu wa Korea Kusini Chung Hong-won amejiuzulu kufuatia kuzama kwa Ferry ya Sewol iliyokuwa na jumla ya abiria 476 wengi wao wakiwa ni wanafunzi na walimu, huko pwani ya kusini ya nchi hiyo wiki iliyopita.
“vilio cha familia za wale ambao bado hawajaonekana vinanikosesha usingizi usiku” alisema Chung Hong-won.
Maafisa wa Korea Kusini wamethibitisha jumla ya watu 187 walipoteza maisha katika ajali hiyo.
Wakati akitoa taarifa ya kujiuzulu alisema kitu sahihi anachotakiwa kufanya sasa ni kuwajibika na kujiuzulu kutokana na kile kilichotokea, na kuomba radhi kwa niaba ya Serikali.
image
Baadhi ya wakazi wa Korea Kusini wakimtazama Waziri mkuu wakati akijiuzulu
Haya ndio maneno ya Mr Chung aliyoyasema kupitia televisheni:
“The right thing for me to do is to take responsibility and resign as a person who is in charge of the cabinet, on behalf of the government, I apologise for many problems from the prevention of the accident to the early handling of the disaster.”
image
Aliongeza: “There have been so many varieties of irregularities that have continued in every corner of our society and practices that have gone wrong. I hope these deep-rooted evils get corrected this time and this kind of accident never happens again.”
Rais Park Geun-hye wa Korea Kusini amekubaliana na kujiuzulu wa waziri mkuu wake.
Source: BBC

Thursday, April 24, 2014

MAIGE "KUWA NA SEREKALI TATU TANZANIA ITAINGIA KATIKA MAAJABU YA DUNIA"

Mjumbe wa Bunge la Katiba, Almas Maige amesema endapo wajumbe wa Bunge hilo watapitisha muundo wa Serikali tatu, nchi itaingia katika kitabu cha maajabu ya dunia cha Guiness Book of Records.

“Hili litakuwa shirikisho la pekee hapa duniani lenye marais wengi katika nchi mbili, linaweza kuingia katika kitabu cha maajabu cha Guiness kwa kuwa na marais wengi katika nchi maskini sana,” alisema.

Mjumbe huyo alisema amejaribu kufuatilia hoja za wanaounga mkono muundo huo na kufananisha na nchi za Marekani na Nigeria, lakini akasema katika nchi hizo Rais wa nchi ni mmoja.

“Mimi nimejaribu kuwafuata wanaofananisha na Marekani na Nigeria, wameshindwa kusema katika nchi hizo mbili Rais ni mmoja tu hakuna wingi wa Rais kutokana na majimbo,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, mjumbe huyo aliwashangaa wajumbe wanaotokana na kundi la Ukawa kujigeuza kuwa wachunguzi wa kijinai kwa kuhoji uhalali wa saini ya muasisi wa Muungano, Abeid Aman Karume.

“Mimi nawashangaa sana wanasiasa hawa na wanasheria wa Ukawa wamejigeuza Forensic Expert (wachunguzi wa jinai). Mimi ningewaunga mkono kama wangeenda kuwauliza watoto wa marehemu,” alisema.

Aliongeza kusema: “Watoto wa marehemu wapo Zanzibar… Yupo Aman Karume aliyekuwa Rais wa Zanzibar na yuko Balozi Ali Karume na yuko pia mama Karume. Kwa nini hawawaulizi,” alihoji.

“Mimi ningefurahi sana kama wangeenda kuwauliza wanafamilia sahihi hii ni ya baba yenu? Au je, mheshimiwa mama hii ni sahihi ya mumeo? Wangekataa ndipo tungewaunga mkono,” alisisitiza.

Mjumbe huyo alisema kinyume chake, Ukawa wanavaa gamba la elimu ambayo hawana na vilevile hawajui maana na tafsiri sahihi iliyoandikwa miaka 50 iliyopita.

“Taaluma ya sasa ingeweza kugundua wino uliotumika una umri gani na kuondoa kero hiyo kama ni ya juzi au jana au kama imeghushiwa,” alisema mjumbe huyo na kuongeza kusema:

“Wataalamu wa Forensic (uchunguzi wa kijinai) wangeweza kugundua wino huo una miaka 50. Wanafanya kitu ambacho hawakijui na wanadhalilisha Watanzania.”

Mjumbe huyo alisema yeye anaunga mkono muundo wa Muungano wa Serikali mbili na kuwa Serikali tatu ni sawa na mtu kunywa sumu.